USIMAMIZI
Ofisi ya Msajili wa Hazina ina wajibu wa kuangalia kwa ukaribu shughuli za uwekezaji wa umma, ikiwa ni pamoja na kufuatilia na kutathmini utendaji, kuweka malengo ya kifedha, na kuidhinisha mipango ya kimkakati na kanuni.
Ili kuhakikisha usimamizi bora wa mali na uwekezaji mwingine wowote ulio chini ya mamlaka yake, Msajili wa Hazina atafuatilia kwa karibu na kudhibiti masuala ya Mashirika ya Umma na Mashirika ya Kisheria, na hasa, anaweza:
(a) Kuchanganua ripoti za mara kwa mara na za mwaka;
(b) Kutathmini bajeti za kila mwaka;
(c) Kufanya tathimini ya utendaji;
Waziri mwenye dhamana anaweza kuandaa kanuni zitakazobainisha taratibu zinazohitajika kwa ajili ya utekelezaji bora na wenye ufanisi wa mamlaka, udhibiti, na uangalizi unaotolewa kwa Msajili wa Hazina.