Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

OFISI YA MSAJILI WA HAZINA

Ofisi ya Msajili wa Hazina ina jukumu la kusimamia ubinafsishaji wa mali za umma, usimamizi na ufuatiliaji wa mashirika ya umma, ukusanyaji wa madeni ya Serikali yaliyorithiwa kutoka CHC, na urekebishaji na ufilisi wa mali zisizozalisha faida katika kampuni au mashirika yaliyobinafsishwa

Kama jukumu muhimu la Ofisi ya Msajili wa Hazina, ubinafsishaji unahitaji ufuatiliaji na tathmini ya taasisi zilizo binafsishwa na Serikali ili kuhakikisha kuwa kuna ufanisi na utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa kati ya Serikali na wawekezaji/wanunuzi kwa wakati maalum.

Hadi sasa, kuna jumla ya taasisi 341 zilizobinafsishwa na zinafuatiliwa na Msajili wa Hazina, ambapo 159 ni viwanda, 109 ni makampuni, na 73 ni mashamba.