Ushauri
Ofisi ya Msajili wa Hazina ina jukumu la kutoa ushauri kwa Serikali kuhusiana na kuanzishwa kwa mashirika ya umma na mashirika ya kisheria. Ushauri huo unalenga kuboresha utendaji wao.
Ofisi ya Msajili wa Hazina ina jukumu la kutoa ushauri kwa serikali kuhusu kuanzishwa kwa Mashirika ya Umma na Mashirika ya Kisheria (PSCs), lengo likiwa ni kupendekeza hatua za kuboresha utendaji na ufanisi wa kiutendaji wa mashirika hayo.
Katika kuanzisha PSCs, Rais anaweza kumtaka Msajili wa Hazina kumshauri kuhusu;
(a) malengo ya shirika linalokusudiwa baada ya kushirikiana na wizara husika;
(b) faida za kuanzisha shirika hilo pamoja na changamoto na hatari zinazoweza kutokea katika kuanzishwa kwa shirika hilo;
(c) upatikanaji wa fedha zinazohitajika kwa ajili ya kuanzishwa kwa shirika hilo;
(d) mtaji wa hisa unaohitajika;
(e) idadi ya hisa ambazo serikali itazisajili; na
(f) njia ya ugawaji wa hisa, ikiwa zipo.
Vilevile, Msajili wa Hazina anatekeleza jukumu la ushauri katika kuamua mabadiliko ya kimpangilio yanahitajika katika shirika la umma, na kusaidia katika mwelekeo wa uamuzi wa Rais wa kuboresha mashirika ambayo hayatekelezi vyema majukumu yao.
Pale ambapo Rais, kwa ushauri wa Msajili wa Hazina, ataridhika kuwa Shirika la Umma au la Kisheria linalomilikiwa na Serikali halifanyi kazi yoyote kwa ufanisi, Rais anaweza;
(a) kutangaza kuwa shirika lililopo litakoma kuwepo au litakoma kutekeleza baadhi ya majukumu au yote;
(b) kuhamisha mali au madeni ya shirika lililopo kwa Shirika la Umma au Kisheria, kama inavyostahili;
(c) Pale ambapo Rais atatangaza kuwa Shirika la Umma au la Kisheria limeacha kutekeleza kazi yoyote, itakuwa ni kinyume cha sheria kwa shirika hilo kutekeleza kazi hiyo.