Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

OFISI YA MSAJILI WA HAZINA

Ofisi ya Msajili wa Hazina kuhamishiwa Morocco Square
15 Feb, 2025
Ofisi ya Msajili wa Hazina kuhamishiwa Morocco Square

Na mwandishi wa OMH

Dar es Salaam. Ofisi ya Msajili wa Hazina imetangaza mpango wake wa kuhamia jengo la Morocco Square ‘Treasury Registrar Tower’, lililopo Kinondoni, jijini hapa, ifikapo Machi 1 mwaka huu.

Kwa sasa, Ofisi za Msajili wa Hazina zipo katika majengo ya CHC Mtaa wa 50 Mirambo na 33 Samora, Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Msajili wa Hazina, Bw. Nehemiah Mchechu, katika jengo jipya Ofisi ya Msajili wa Hazina itachukua ghorofa ya 16-19.

Alisema mabadiliko hayo hayataathiri shughuli za Ofisi ya Msajili wa Hazina kwani zitaendelea kupatikana kama kawaida, kuanzia saa 1.30 asubuhi hadi saa 9.30 alasiri.

“Uamuzi wa kuhamisha ofisi unalenga kuboresha mazingira ya kufanyia kazi na hivyo kuongeza ufanisi wa Ofisi ya Msajili wa Hazina,” alisema Bw. Mchechu katika taarifa yake kwa umma.