UKAGUZI WA NDANI

MAJUKUMU NA UTENDAJI WA KITENGO 

Kipengele 28 cha kanuni za fedha za umma (2004) na mwongozo wa ukaguzi wa ndani kipengele cha 2.3 wa mwaka 2013 inamtaka Afisa Masuuri kuanzisha kitengo cha ukaguzi wa ndani. Madhumuni ya kitengo hiki ni kutoa ushauri kwa Afisa Masuuli juu ya utumiaji mzuri wa rasilimali. Majukumu hayo ni kama ifuatavyo:-

 1. Kukagua na kutoa taarifa kama kuna udhibiti wa kutosha kwenye makusanyo, utunzaji na matumizi ya rasilimali fedha za ofisi.
 2. Kukagua na kutoa taarifa kama mifumo ya utendaji iliyo ainishwa kwenye sheria ,kanuni na maelekezo mbalimbali toka kwa Mhasibu Mkuu wa Serikali yanafuatwa ili kuhakikisha kuwa kuna udhibiti wa kutosha kwenye matumizi fedha katika ofisi.
 3. Kukagua na kutoa taarifa kama mipangilio na mgawanyo kwenye akaunti za mapato (revenue) na matumizi ni sahihi.
 4. Kukagua na kutoa taarifa juu ya usahihi wa hesabu na tarifa mbalimbali zinazo andaliwa na ofisi.
 5. Kukagua na kutoa taarifa juu ya mifumo iliopo na inayotumika kutunza mali za serikali, pamoja na kufanya uhakiki wa mali hizo.
 6. Kupitia na kutoa taarifa juu ya shughuli au mipango ya ofisi ilki kuona kama inaendana na malengo na madhumuni ya uanzishwaji wa ofisi.
 7. Kupitia na kutoa taarifa juu ya hatua mbalimbali zilizo chukuliwa na menajimenti katika kujibu hoja za Mkaguzi wa ndani;na kusaidia manajimenti juu ya utekelezaji wa mapendekezo ya hoja hizo;na pale inapofaa kusaidia namna ya utekelezaji wa mapendekezo yaliyotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.
 8. Kukagua mifumo ya TEKNOHAMA iliyopo katika ofisi na kutoa taarifa kama kuna umadhubuti wa udhibiti uliopo.
 9. Kuandaa Mpango kazi na Mpango mkakati wa ukaguzi
 10. Kuandaa na kusimamia mipango ya ukaguzi
 11. Kufanya ukaguzi wa thamani kwenye miradi ya kimaendeleo na kaguzi za thamani mbalimbali