MENEJIMENTI YA USIMAMIZI WA UNUNUZI

MAJUKUMU YA KITENGO CHA UNUNUZI

Kitengo cha Menejimenti ya Ununuzi (PMU) ni moja ya vitengo vilivyopo katika Ofisi ya Msajili wa Hazina ambacho kina wajibu wa kusimamia unununi kwa mujibu wa sheria ya ununuzi ya Umma Na. 7 ya mwaka 2011 na kanuni zake za mwaka 2013.

Kwa mujibu wa Muundo wa Ofisi ya Msajili wa Hazina (Organisation Structure) na Sheria ya Ununuzi ya Umma Na.7 ya mwaka 2011 na Kanuni zake za mwaka 2013. Kitengo cha Menejimenti ya Ununuzi kina majukumu yafuatayo:-

 1. Kusimamia majukumu yote ya ununuzi na Uuzaji kwa njia ya zabuni;
 2. Kusaidia kazi zinafanywa na bodi ya zabuni;
 3. Kutekeleza maamuzi ya bodi ya zabuni;
 4. Kuandaa mpango wa ununuzi na kusimamia utekelezaji wake;
 5. Kuangalia na kuandaa taarifa ya mahitaji;
 6. Kuandaa matangazo ya zabuni;
 7. Kuandaa hati ya zabuni na taarifa yake;
 8. Kutoa mikataba iliyo idhinishwa kwa wazabuni;
 9. Kutunza na kuifadhi kumbukumbu ya ununuzi na uuzaji;
 10. Kuanda na kuhifadhi rejista ya mikataba ya wazubuni wanaoshinda zabuni; na
 11. Kuandaa taarifa za kila wakati zinazo fanyika katika stoo kuwezesha uhakiki wa mali na utunzaji katika stoo.