TEKNOHAMA

MAJUKUMU

Katika kufanikisha majukumu ya ofisi na kufikia malengo iliyojiwekea, Kitengo cha Teknohama kinawajibika kutekeleza majukumu yafuatayo ;-

  1. Kutekeleza Sera ya Teknohama ya Serikali,
  2. Kubuni na kushauri Ofisi kuhusiana na Mifumo yote ya Teknohama kwa ndani ili kuboresha utendaji;
  3. Kuendeleza na Kuratibu Mfumo Mtambuka wa Taarifa za Mashirika yaliyoratibiwa shughuli zake na Ofisi ya Msajili wa Hazina,
  4. Kuratibu na Kushauri matumizi bora ya vifaa na program za ofisi ,
  5. Kushauri na kusaidia ununuzi wa programu na vifaa vya Kiteknohama katika ofisi,
  6. Kuanzisha na Kuratibu matumizi sahihi ya mawasiliano kwa ndani na nje ya ofisi;
  7. Kufanya tafiti na kupendekeza maeneo ya kutumia Teknohama kama chombo cha kuboresha utoaji wa huduma kwa mashirika na Taasisi za Umma;
  8. Kukuza matumizi ya Teknohama katika Mashirika na Taasisi za Umma na;
  9. Kuboresha Mawasiliano ya Ofisi kwa wadau wake kupitia wavuti yake