MIPANGO

Kazi kubwa ya Kitengo cha Mipango ni kusimamia na kuratibu mipango na Bajeti ya Ofisi ya Msajili wa Hazina. Aidha, kulingana na muundo wa Ofisi kitengo kina majukumu yafuatayo:

 1. Kuratibu matayarisho ya Bajeti,Mpango wa mwaka pamoja na kufuatilia utekelezaji;
 2. Kusimamia ufuatiliaji na tathmini wa Shughuli za Msajili wa Hazina;
 3. Kuandaa michango ya Ofisi katika Hotuba ya Bajeti pamoja na taarifa ya mwaka ya Uchumi;
 4. Kuwajengea uwezo watumishi katika maeneo ya Mpango Mkakati, bajeti na mfumo wa ufuatiliaji na tathmini;
 5. Kuratibu mapitio ya Sera za Ofisi ya Msajili wa Hazina na kuzihuisha ili ziendane na Sera za kitaifa;
 6. Kupitia na kutoa ushauri juu nyaraka mbali mbali za kisera kutoka kwenye mashirika na Taasisi za Umma;
 7. Kutayarisha makubaliano ya Awali (MOU) kwenye miradi/Programu ili kupata fedha za nje;
 8. Kuratibu shughuli za Bunge zinazohusu utendaji wa Mashirika na Taasisi za Umma;
 9. Kutayarisha miradi ya Ofisi ya Msajili wa Hazina, Mpango kazi na kufuatilia utekelezaji wake;
 10. Kuibua mikakati ya kutafuta rasilimali fedha za kuendesha Ofisi;
 11. Kufanya utafiti wa awali kuhusu utoaji wa huduma ili kupata maoni ya wadau juu ya huduma zitolewazo na kuishauri menejimenti; na
 12. Kuratibu mapitio ya utendaji wa nusu mwaka na wa mwaka wa Ofisi ya Msajili wa Hazina .