MAJUKUMU YA OFISI

 1. Kusimamia na kutathmini utendaji kazi wa Mashirika na Taasisi za Serikali kwa kuzingatia vigezo vya utendaji kazi vilivyowekwa;
 2. Kusimamia hisa za Serikali katika Makampuni na Mashirika ya Umma;
 3. Kushauri kuhusu kuanzisha Mashirika mapya ya Umma, kuyaunganisha, kuyauza au kuyavunja kwa madhumuni ya kuleta ufanisi na kushauri jinsi ya kuyasaidia mashirika yenye matatizo ya kipekee;
 4. Kuweka malengo ya kifedha na viwango au vigezo vya utendaji kazi (Performance Indicators) ambavyo vitazingatiwa na Taasisi na Mashirika ya Umma na Taasisi;
 5. Kuthibitisha teuzi za Wakurugenzi wa Bodi na kutathmini ufanisi wao na kupendekeza Serikalini mbinu za kuboresha utendaji wao wa kazi;
 6. Kuweka au kuondoa rasilimali ya mtaji katika Mashirika ya Umma baada ya kushauriana na Serikali;
 7. Kukusanya gawio (dividend) kutoka katika Mashirika ya Umma ambako Serikali imewekeza mitaji ya hisa;
 8. Kuidhinisha Kanuni za Fedha katika Mashirika ya Umma;
 9. Kuidhinisha Muundo wa Taasisi, Miundo ya Utumishi, Kanuni za Utumishi, Mikataba ya hiyari, mishahara na marupurupu ya wafanyakazi wa Mashirika na Taasisi za umma yanayozingatia tija, ufanisi, kukua kwa mtaji (wekezo) na kulipwa kwa gawio na ziada Serikalini;
 10. Kusimamia na kufanya tathmini ya mipango, bajeti na malengo ya mwaka kwa taasisi na Mashirika ya Umma;
 11. Kusimamia mfuko wa uwekezaji katika Mashirika ya Umma;
 12. Kufanya tathmini ya mara kwa mara ya utendaji kazi na ufanisi wa pamoja kati ya kamati za uongozi za Taasisi na Mashirkia ya Umma, na kutoa mapendekezo ya namna ya kuboresha utendaji kazi wa Bodi na Kamati hizo;
 13. Kufuatilia na kufanya tathmini ya mipango ya mafunzo katika Taasisi na Mashirika ya Umma;
 14. Kufuatilia Mitaji (capital Grants and Capital Funds), Ruzuku, au retained earnings katika Mashirika na uwekezaji mwingine wa Umma;
 15. Kuandaa na kutoa Nyaraka na Miongozo mbalimbali ili kuleta na kuongeza tija na ufanisi katika Taasisi na Mashirika ya Ummma;
 16. Kusimamia na kutoa idhini kwa Taasisi na Mashirika ya Umma yanayotaka kuwekeza katika Mashirika mengine;
 17. Kutathmini na kutoa taarifa za uwekezaji katika Taasisi na Mashirika ya Umma kwa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mwaka;
 18. Kusimamia zoezi la urekebishaji na ubinafsishaji wa Mashirika ya Umma.